Sunday, December 22, 2024

Gigy Money Afunguka Kuhusu Hisia Zake na Mapenzi

Gigy Money Afunguka Kuhusu Hisia Zake na Mapenzi

 

Msanii maarufu wa Bongo, Gigy Money, amefunguka kwa mara nyingine kuhusu maisha yake binafsi na hisia zake za ndani kuhusu mapenzi. Kupitia mazungumzo ya wazi, Gigy alieleza kuwa yeye ni mtu mwenye hisia kali na hawezi kuficha hali yake, hususan linapokuja suala la mapenzi.


Ameeleza kwamba mara ya mwisho alijaribu kukaa muda mrefu bila kushiriki mapenzi ilikuwa kipindi alipoachana na mzazi mwenzake, Mo J, na aliweza kuvumilia kwa wiki moja tu. Hata hivyo, hali hiyo ilianza kumletea changamoto za kihisia, ambapo aliwahi hata kuzungumza mwenyewe bila kujitambua.

Gigy Money

Gigy Money pia aliongeza kuwa kwa sasa, hawezi kukaa zaidi ya siku tatu bila kushiriki mapenzi, kwani hali hiyo huathiri mabadiliko yake ya kihisia ambayo huonekana wazi kwa watu waliomkaribu.


Maisha ya wasanii mara nyingi huwa ya wazi, lakini Gigy anaendelea kuwa mmoja wa watu wanaothubutu kuelezea hali zao bila kuficha, jambo ambalo limewafanya mashabiki wake kumpenda zaidi.

Gigy Money

Je, una maoni gani kuhusu kauli ya Gigy Money? Tuambie kwenye sehemu ya maoni hapa chini!


Kwa habari zaidi za wasanii, Follow page yetu kwa nyimbo mpya na taarifa mpya. @Mziki DL

0 Comments: