Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Aggy Baby, ameibua gumzo kwenye tasnia ya muziki baada ya kutoa kauli nzito akisema hana hofu na msanii maarufu Zuchu. Akitangaza ujio wake wa albamu mpya, Aggy Baby amesema:
"Nakuja na albamu, wasanii mjipange! Simwogopi Zuchu wala simwogopi kwasababu Zuchu anaimba nyimbo za watoto, mimi naimba nyimbo za watu wazima na zenye jumbe za malavidavi."
Kauli hii imeibua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, ambapo mashabiki wameonyesha hisia tofauti kuhusu ujasiri wa Aggy Baby wa kumlinganisha na Zuchu, ambaye ni moja ya wasanii wa kike wenye mafanikio makubwa nchini Tanzania.
![]() |
Aggy Baby |
Aggy Baby anaonekana kujiamini na kujitofautisha na wasanii wengine kwa mtindo wake wa muziki, akisisitiza kuwa nyimbo zake zina ujumbe mzito wa kimapenzi kwa watu wazima. Albamu yake inatarajiwa kuleta ushindani mkubwa kwenye soko la muziki.
Je, unadhani Aggy Baby ataweza kushindana na Zuchu? Tafadhali toa maoni yako!
![]() |
Aggy Baby |
Kwa taarifa zaidi kuhusu ujio wa albamu yake, Kwa habari zaidi za mastaa na burudani, tembelea
Mziki DL - Nyumbani kwa Muziki Bora!
0 Comments:
Post a Comment